Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta amesema amefuzu majaribio kwenye klabu ya CSKA Moscow ya Urusi ila anasubiri majibu ya lini atajiunga nayo.
Samatta aliyekwenda kufanya
majaribio kwa wiki mbili kwenye klabu hiyo ambako alikumbana na balaa la
kuumia enka na kushindwa kucheza baadhi ya mechi, ingawa amesema ana
matumaini ya kufanya vizuri.
Mshambuliaji huyo wa Taifa
Stars alisema maofisa wa CSKA walimwambia kuwa watamtumia majibu ya
majaribio yake kwa njia ya mtandao kati ya jana, Jumamosi ama mwanzoni
mwa wiki ijayo.
“Mambo yalikwenda vizuri, nilifanya
majaribio kwa siku zote kama ilivyopangwa licha ya kwamba nilishindwa
kucheza baadhi ya mechi, nasubiri majibu.
“Maofisa wa
pale na wakala wangu wameniambia kuwa majibu yatatoka kati ya kesho,
Jumamosi ama ndani ya siku hizi mbili, nasubiri na nina imani yatakuwa
mazuri,” alisema Samatta.
Hata hivyo, taarifa
zilizopatikana mjini Lubumbashi zinaeleza kuwa endapo CSKA haitatoa ofa
ya nguvu kuna uwezekano mkubwa mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi akagoma
kumruhusu Samatta hadi mkataba wake utakapomalizika.
No comments:
Post a Comment