
Baada
ya Liverpool na Manchester United kupata ushindi jioni ya leo – vilabu
vingine vikubwa kwenye ligi kuu ya Uingereza Chelsea na Man City navyo
vilikuwa vikichuana katika vita kugombea uongozi wa ligi hiyo.
Mechi hiyo ambayo
ilipigwa jijini London katika dimba la Stamford Bridge imemalizika muda
mfupi uliopita huku Chelsea wakiweza kuendelea kuustawisha uongozi wao
kwenye msimamo wa ligi.
Matokeo
ya mechi hiyo ni sare ya 1-1 ambayo imeendelea kuipa Chelsea uongozi wa
pointi 5 zaidi ya Man City wanaoshika nafasi ya pili.
Chelsea
walianza kufunga goli kupitia Loic Remy ambaye alimalizia kazi nzuri ya
Eden Hazard katika dakika ya 40 – lakini muda mfupi baadae David Silva
akaisawazishia City baada ya kumalizia pasi ya Sergio Aguero.
Mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa yakisomeka 1-1.
No comments:
Post a Comment