KLABU kongwe na tajiri katika Ligi Kuu Bara za Azam FC, Simba na Yanga kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2014-2015, zilitikisa kwenye usajili ambao kila mmoja akiamini amelamba dume.
Lakini baada ya wachezaji hao kuingia mzigoni,
wapo wachezaji ambao unaweza kusema klabu hizo zililamba dume zilipokuwa
zinasajili kutokana na namna waliosajiliwa walivyowasaidia na
wanavyonogesha ushindi wa timu au uchezaji wake. Wachezaji wafuatao
wamefanya kazi ya maana mpaka sasa;
Frank Domayo
Anaendesha gari aina ya Alteza. Ni kiungo wa Azam
FC, alisajiliwa akitokea Yanga mwanzoni mwa msimu huu, lakini
hakufanikiwa kucheza mechi zote za awali kwa sababu ya majeraha ambayo
alifanyiwa upasuaji wa nyama za paja la mguu wa kushoto.
Lakini baada ya kupona na kurudi uwanjani, Domayo amekuwa mtamu kwa Azam kwa sababu ubora wake, umeongezeka maradufu.
Sasa ni mfungaji mzuri, analijua goli vizuri sana
na sehemu ya mabao yake, yameitoa Azam kimasomaso. Kocha wake, Mcameroon
Joseph Omog anajivunia uwepo wa Domayo kikosini hapo kuwa ni mhimili na
ameifanya safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho, kuimarika.
Hassan Ramadhani ‘Kessy’
Ni beki wa kulia wa Simba, yeye amesajiliwa katika
dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar. Tangu atue kikosini hapo, Kessy
amekuwa tegemeo kutokana na namna anavyofanya vizuri.
Ubora wake umedhihirisha hata anapokosekana ni pengo kikosini humo.
Umbo lake ni dogo lakini jamaa ni mtu wa kazi, ana
kasi, nguvu na akili ya mpira, anaijua vizuri kuicheza beki ya kulia
katika kupandisha mashambulizi na kukaba.
Simba haiwezi kujuta na sasa inajisifu kuwa imelamba dume.
Andrey Coutinho
No comments:
Post a Comment