
Mshambulizi
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na
mabingwa mara nne wa kihistoria wa Afrika, TP Mazembe mara baada ya
kumalizika kwa mkataba wake.
Samatta
ambaye alipata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya CSKA Moscow
ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa nyingi barani ulaya na kama
ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi
zaidi barani Afrika.
Hivi
karibuni kuna vyombo vya habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo
ana furaha kuendelea kuichezea TP lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.
”
Sina furaha hapa ( TP mazembe) nitaondoka wakati wa majira ya usajili
katikati ya mwaka na sitaongeza mkataba” anasema Samatta, ni wapi
anakwenda, nini kinachomuondoa TP Mazembe,

Haya hapa mahojiano kati ya Mbwana Samatta na Mwandishi wa mtandao huu.
MWANDISHI;
Samatta kumekuwa na taarifa kwamba licha ya baadhi ya vikwazo
unavyokutana navyo unapopata fursa ya kucheza Ulaya katika klabu yako ya
TP Mazembe bado unafurahia kuwepo ndani ya timu hiyo. Je, ni kweli una
furaha kuendelea kuichezea TP?
MBWANA SAMATTA; Hahaha, ni uongo huo, sina furaha kuendelea kucheza hapa na
wala sitaongeza mkataba mpya, nadhani nitaondoka wakati wa usajili ujao
wa kiangazi.
MWANDISHI; Kwa niaba ya wasomaji wa webisite hii (www.shaffihdauda.co.tz)
ningependa kufahamu nini kilitokea katika majaribio yako CSKA Moscow ya
Urusi klabu ambayo ilikupatia nafasi ya kwenda kufanya majaribio. Ni
kweli sababu za majeraha ndiyo zimekunyima nafasi?
MBWANA SAMATTA; Kwa kweli suala la majeraha lilikuwa ni sababu ndogo sana na
mahitaji ya CSKA, lakini tatizo lilikuja katika suala la makubaliano
kati ya CSKA na TP. Kiukweli Mazembe walihitaji kiasi kikubwa sana
ambacho ambacho ni vigumu kwa klabu ya ulaya kutoa kwa mchezaji
anayecheza Afrika.
Ukichanganya
na sababu za kimkataba ambao umebaki mwaka mmoja kati yangu na TP
ilibidi CSKA washindwe kwa sababu hizo na si majeraha kwa kuwa
walinihati hivyohivyo. Baada ya hapo nilizungumza na klabu kuhusu ‘
future’ yangu, so nasubiri muda ukifika nitaingia nao makubaliano flani
hata kabla muda wangu haujakwisha na TP.
MBWANA SAMATTA; Nafasi ipo ya mimi kujiunga na CSKA pia bosi wa klabu hiyo
amekuwa na urafiki na klabu nyingi za ulaya hivyo kuna uwezekano mkubwa
akaninunua kwa sababu ya klabu nyingine, nadhani umenielewa.
MWANDISHI; Kwa nini unaondoka TP Mazembe?
MBWANA SAMATTA; Nadhani imetosha kwa sisi kuendelea kucheza barani Afrika, sasa nataka kuishi katika ndoto zangu.
MWANDISHI; Kila mwanasoka huwa na ndoto kubwa, ndoto yako imeegemea wapi kimpira?
MBWANA SAMATTA; Napenda kucheza LIGA BBVA, ndoto yangu ni kucheza ligi kuu ya Hispania, La Liga.
MWANDISHI; Miaka minne ndani ya klabu kubwa Afrika TP Mazembe imekufunza nini ukizingatia ulitoka Tanzania ukiwa U18?
MBWANA SAMATTA; Kwa kweli nimepevuka kwa kiasi kikubwa kimpira na kiakili,
tayari nimecheza dhidi ya klabu zote kubwa barani Afrika. Nimepata
uzoefu mkubwa sana na kujiamini kwa kiasi kikubwa. Nashukuru kwa kila
kitu ambacho TP wamekuwa wakiendelea kufanya dhidi yangu.
Nimejiiimarisha kutoka mchezaji kijana hadi kuwa mtu jasiri ndani ya
uwanja.
MWANDISHI; Je, umezungumza na mmiliki wa TP, Moise Katumbi kuhusu kuondoka kwako kabla ya kumalizika kwa mkataba, amesemaje?
MBWANA SAMATTA; Nilizungumza naye sana tu na amekubaliana name hivyo muda
utakapofika amesema hatokuwa na kipingamizi tena, ataruhusu niondoke.
No comments:
Post a Comment