MSHAMBULIAJI
Mbwana Ally Samatta amerejea jana mjini Lubumbashi kuendelea na maisha
chini ya utawala wa Moise Katumbi Chapwe, rais wa klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Samatta akiwa na
Mtanzania mwenzake anayecheza naye Mazembe, Thomas Ulimwengu wamepiga
picha na mmoja wa Wakurugenzi wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam iliyo
ziarani Lubumbashi, Jamal Bakhresa.
Na jamal Bakhresa ameituma picha hiyo BIN ZUBEIRY jana akisema amefurahi kukutana na vijana na kuzungumza nao mawili matatu.

Mbwana Samatta kulia akiwa na Jamal Bakhresa na Thomas Ulimwengu kushoto jana mjini Lubumbashi
Habari zaidi kutoka
Lubumbashi zinasema kwamba, klabu ya CSKA Moscow ya Urusi iliamua
kuachana na Samatta kwa sasa baada ya kuumia enka akiwa katika wiki ya
kwanza ya majaribio.
Kiongozi mmoja wa Mazembe
ambaye hakupenda kutajwa jina, ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba
timu hiyo ya Ulaya ilivutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo wa Tanzania,
lakini ilishindwa kumtathmini zaidi baada ya kuumia.
Hata hivyo, amesema klabu
(TP Mazembe) chini ya Rais, Moise Katumbi bado wapo bega kwa bega
kuhakikisha wanatimiza ndoto za mtoto wa Mbagala, Samatta kucheza Ulaya
kwa maslahi makubwa.
Mapema mwezi huu, Samatta
alipata fursa ya kufanya mazoezi na klabu ya CSKA Moscow ya Urusi
ambayo ilikuwa inamjaribu kwa ajili ya kumnunua, hata hivyo bahati mbaya
kwake aliumia enka.
Samatta ambaye amebakiza
mwaka mmoja katika Mkataba wake TP Mazembe tangu asajiliwe kutoka Simba
SC ya Dar es Salaam, alipania mno Januari hii kuhamia Ulaya, lakini
inaonekana wakati wake bado
No comments:
Post a Comment