Van Gaal apiga hesabu - TodayNews

Breaking

Tuesday, 6 January 2015

Van Gaal apiga hesabu



      KOCHA wa Manchester United, Louis vanGaal amedai kucheza mechi mbili ndani ya saa 48 kumewachosha wachezaji wake na kushindwa kupata ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu England juzi Jumapili.
Man United ilitoka sare ya bila kufungana na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika White Hart Lane juzi ikiwa ni saa 48 tu kupita tangu ilipocheza dhidi yaNewcastle United kwenye ligi hiyo.
Hata hivyo, Mdachi huyo bado anaamini kikosi chake kitabeba ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu licha ya kushindwa kupunguza pengo la pointi baina yake na timu mbili za juu.
Kwa matokeo hayo, Man United sasa imeachwa na vinara Chelsea kwa tofauti ya pointi 10 na pointi saba dhidi ya Manchester City ambazo timu hizo mbili nazo zilitoka sare katika michezo yao ya wikiendi.
Van Gaal alisema: “Bado naamini kwa sababu kiwango chetu kimekuwa kikikuwa kila wiki. Ndiyo hivyo, tutakuwa wazuri zaidi 2015. Subiri tu kuona.”
Kocha huyo aliwageukia mastraika wake na kuwaeleza kwamba kama wanataka kunyakua ubingwa, basi ni lazima watimize wajibu wao wa ndani ya uwanja ambao ni kutumia ipasavyo nafasi wanazozipata. Kwenye mechi dhidi ya Spurs, washambuliaji wa Man United walipoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment