Azam FC itakutana na Mtibwa Sugar katika Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi keshokutwa kufuatia kumaliza nafasiya pili katika Kundi B, nyuma ya mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda.
Azam FC imeshinda 1-0 katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B dhidi ya Mtende Rangers uliofanyika Uwanjawa Amaan, Zanzibar jioni ya leo.
Hadi mapumziko, Azam FC walikuwa tayari wamekwishapata bao hilo lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa waBurundi, Didier Kavumbangu dakika ya 34 akimalizia krosi ya winga wa kimataifa wa Uganda, Brian Majwega.
Kavumbangu alifunga bao hilo kiasi cha dakika nane tangu aingie uwanjani kwenda kuchukua nafasi ya Kelvin Fridayambaye mchezo ulimkataa leo na kocha Joseph Marius Omog akaamua kumpumzisha mapema.
Katika mechi zilizotangulia, mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda waliwafunga KMKM 2-1 mchezo wa Kundi B, wakatiPolisi iligawana pointi na Taifa Jang’ombe kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Mao dze Tung.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Serge Wawa, MudathirYahya/Shomary Kapombe dk, Frank Domayo, Brian Majwega, Himid Mao/Farid Mussa dk70, John Bocco/AmriKiemba dk78na Kelvin Friday/Didier Kavumbangu dk26.
Mtende Rangers; Juma Machano, Suleiman Juma, Amour Hajji, Ali Mohammed, Mussa Said, Suleiman Said, TwahaRajab, Ujata Makoba/Herman Kunambi dk59, Jumanne Seif, Saleh Ahmed/Abeid Salum dk66 na Mussa Digubike.
No comments:
Post a Comment