Mtoto wa Ronaldo hajatulia - TodayNews

Breaking

Tuesday, 6 January 2015

Mtoto wa Ronaldo hajatulia



      MTOTO wa straika wa zamani wa Brazil, Ronaldo de Lima ameingia kwenye kashfa baada ya kuonekana akibusiana na mwalimu wa chekechea katika ukumbi wa starehe za usiku.
Mtoto huyo, Ronald Ronaldo mwenye umri wa miaka 14 tu, ameripotiwa kufanya kazi ya kuwa DJ katika klabu hiyo ya starehe za usiku.
Picha ilimwonyesha mtoto huyo akibusiana na mwalimu huyo wa kike mwenye umri wa miaka 27 ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa karibu wiki nzima, lakini mrembo Lu Bernardi, alisema kwamba Ronald alimwambia kwamba ana umri wa miaka 18.
“Naapa sikufahamu. Tulipokutana klabu, alionekana kuwa mrefu kuliko wote. Unawezaje kudhani kijana mwenye urefu wa mita 1.85 kuwa ni bado kinda?” alisema mrembo Lu.
“Alinidanganya kwamba ana miaka 18. Naapa sikuutilia shaka umri wake.”

No comments:

Post a Comment