Coutinho: Maximo angenipoteza, sasa ninafuraha Yanga - TodayNews

Breaking

Tuesday, 6 January 2015

Coutinho: Maximo angenipoteza, sasa ninafuraha Yanga



    MSIKIE kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, anachosema kwamba anafurahishwa na mfumo wa sasa wa timu yao chini ya kocha Hans Van Der Pluijm kwani unamfanya aonekane bora uwanjani tofauti na alipokuwa chini ya Mbrazili mwenzake, Marcio Maximo.
Coutinho aliliambia Mwanaspoti kuwa soka la kuzuia wakati wa Maximo lilikuwa linampa tabu na hakuufurahia mfumo huo tofauti na sasa ambapo amepewa uhuru wa kucheza kwa kushambulia.
Alisema hakuwa na amani wakati Yanga ilipokuwa chini ya Maximo kwani alikuwa anajua safari ya kurudi kwao Brazil inaweza kumkuta muda wowote kwa kuwa angeonekana wa kawaida uwanjani kama ilivyokuwa kwa Genilson Santos ‘Jaja’ ambaye pia aliponzwa na mfumo wa kuzuia.
“Sikuwahi kufurahia soka wakati nipo na Maximo hapa Yanga, kwani tulikuwa tunacheza kwa kuzuia na sikupata muda mwingi wa kushambulia kwa uhuru na kazi ilikuwa kubwa ya kushuka kuzuia na wakati huohuo mpandishe mashambulizi,” alisema.
“Nilijua thamani yangu ya ufungaji haitaweza kuonekana na kwa jinsi mashabiki na viongozi wa Yanga wanavyotaka mafanikio haraka nikajua naweza kurudishwa nyumbani muda wowote hivyo nilijiona soka langu linaisha taratibu na sikuweza kubadili mfumo wa kocha.”
Alisema mara zote alikuwa anaishi kwa mawazo hasa baada ya Jaja kujiondoa klabuni na alihisi kipaji chake kitapotea kwa kucheza kwa kujilinda muda mwingi kuliko kushambulia.
Juzi Jumapili katika mchezo dhidi ya Polisi Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi, Coutinho aliifungia Yanga mabao mawili akichangia ushindi wa mabao 4-0.
“Lakini sasa naishi kwa amani kwani Pluijm alizungumza nami na kunitaka nicheze kwa kushambulia,” a

No comments:

Post a Comment