MOURINHO ATOA SABABU HIZI KUU 3 ZA UKWELI NA PICHA KAMILI ZILIZOIFANYA MA U KUTOSHINDA MECHI ZIDI YA MAN CITY - TodayNews

Breaking

Sunday, 11 September 2016

MOURINHO ATOA SABABU HIZI KUU 3 ZA UKWELI NA PICHA KAMILI ZILIZOIFANYA MA U KUTOSHINDA MECHI ZIDI YA MAN CITY

mourinho

Katika mahojiano yake mengine na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wa Man U zidi ya Man City Mourinho alitoa sababu kuu 3 zilizowafanya wao kutoshinda mechi zidi ya Man City, Sababu hizo ni;


1. Kucheza chini ya kiwango katika dakika 35 za kipindi cha kwanza

Mourinho akiri kuwa kikosi chake kwa dakika 35 za kwanza kilicheza chini ya kiwango na kuifanya Man City kutawala mechi kwa asilimia zote kitu ambacho kocha huyo anaamini kuwa lazima wawe mbele kiushindi katika dakika hizo. Mourinho pia anaamini gori walilopata wao katika kipindi hicho ilikuwa ni makosa tu ya ulinzi wa Man City.

mourinho & pepe

2. Makosa 2 ya penati aliyoyapuuza refa wa mchezo huo katika kipindi cha pili

.Mourinho alisema kuwa katika kipindi cha pili kipa wa Man City aliweza kumchezea ndivyo sivyo Rooney kosa ambalo alitakiwa kipa huyo apate kadi nyekundu na penati kama ilivyoonyeshwa hapa chini lakini refa huyo alipuuzia.


rooney

.Pili beki wa Man City aliweza kugusa mpira katika kiwiko chake cha mkono na ni kadi ya njano pamoja na penati lakini muamuzi wa mchezo huo alipuuzia kama inavyoonekana hapa chini.


penati


3. Baadhi ya wachezaji kutoimiri vyema kasi ya mchezo katika timu kubwa kitu ambacho Mourinho anaamini kuwa ni kosa lake na atakifanyia marekebisho katika mechi nyingine kubwa zijazo.

Kutokana na hayo Mourinho anaamini kutoshinda kwao ni kosa la refa wa mchezo huo kutoamua maamuzi sahihi kama ilivyoelezwa hapo juu, wachezaji wake kuwa katika kiwango cha chini katika kipindi cha kwanza pia yeye mwenyewe Mourinho kuweka baadhi ya wachezaji wasioweza kuhimiri kasi ya mchezo kwa timu kubwa kama Man City.

No comments:

Post a Comment