JE ARSENAL ITATWAA UBINGWA WA EPL MSIMU HUU? PETR CECH YEYE IMANI YAKE IPO HAPA… - TodayNews

Breaking

Thursday, 24 December 2015

JE ARSENAL ITATWAA UBINGWA WA EPL MSIMU HUU? PETR CECH YEYE IMANI YAKE IPO HAPA…

Petr 4
Golikipa Petr Cech wa klabu ya Arsenal ya England amesema msimu huu klabu yao itaenda mbali zaidi hata kutwaa ubingwa wa ligi kuu kutokana na ari na kikosi imara walichonacho hivi sasa.
Arsenal ambao wako nyuma ya vinara Leicester City kwa points 2, wamepoteza mechi moja tu kati ya 11 walizocheza kwenye ligi mfululizo hadi sasa.
Cech mwenye miaka 33 ameiambia BBC kuwa klabu hiyo itanufaika zaidi pindi wachezaji wake wote walio majeruhi watakapopona na kuwa sawa na hivyo kumpa mwanya mkubwa meneja wao Arsene Wenger kupanga timu atakavyo.
Arsenal ambao ni mabingwa watetezi wa FA Cup walimaliza nafasi ya tatu msimu uliopita wakiachwa kwa points 12 na mabingwa Chelsea, hivi sasa wako katika hali nzuri zaidi sanjari na kuwa na majeruhi.
Petr Cech aliyesajiliwa kwa paundi 10m kutoka Chelsea msimu huu anasema kuwa kuna mambo hayawezi kwenda watakavyo kirahisi, na kwamba suala la mejeruhi haliepukiki, lakini ujio wa wachezaji hao utainufaisha klabu yao katika mbio za ubingwa.
Arsenal msimu huu imekua na wimbi kubwa la majeruhi ambapo hadi sasa wachezaji Jack Wilshere, Dany Welbeck, Francis Coquelini na Tomas Rosicky wote bado ni wagonjwa.

No comments:

Post a Comment