Simba yaichapa Azam 2-1 - TodayNews

Breaking

Sunday, 3 May 2015

Simba yaichapa Azam 2-1

9
  
 Simba ya Jijini Dr es salaam leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Azam FC, katika mtanange uliokuwa wa kusaka nafasi ya pili kunako msimo wa ligi kuu ya Tanzania bara ambayo inaelekea ukingoni.
Katika mchezo huo uliopigwa Taifa , Simba ndio walianza kupata bao lakini halikudumu baada ya muda mfupi kusawazishwa kabla ya Singano kumaliza kazi kwa kufunga bao la pili na la ushindi.
Dakika ya kwanza Azam wanapata free kick ambayo inapigwa na Majwega lakini inakuwa mboga kwa Ivo Mapunda kufatia Kipre Tchetche kufanyiwa madhambi.
Dakika 27 Frank Domayo anakosa bao baada ya mwamuzi wa pembeni kumnyoshea kipendera kuwa kaotea.
Dakika ya 39 Salum Abubakar anapewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Mohamed Hussein licha ya kuwa awali alipewa kadi ya Njano kwa kosa kama hilo.
Azam wanakosa bao dakika ya 45 baada Majwega kushindwa kupiga mpira safi wa krosi iliyochoongwa na Frank Domayo.
Azam wanampumzisha Frank Domayo katika dakika ya 49 kipindi cha kwanza na nafasi yake inachukuliwa na Brison Mariki.
Dakika ya 48 kipindi cha pili Ibrahim Ajibu anaifungia bao la kwanza Simba baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa kutoka winga ya kulia.
Dkika ya 58 Azam FC wanasawazisha bao kupitia kwa Mudadhiru Yahaya akipokea pasi safi ya Kipre Tchetcehe.
Dakika ya 74 Simba wanaongeza bao la pili kupitia kwa Ramadhani Singano baada ya mpira wa kona.
Kufatia ushindi huo sasa Simba wanakuwa wamefikisha pointi 44 ikibakia katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam wenye alama 45.
Ili kujihakikishia nafasi ya pili Simba wanatakiwa kushinda mchezo wa Mwisho huku wakiomba mabaya kwa Azam iweze kupoteza katika mchezo dhido ya Yanga pamoja na Mgambo JKT wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment