Ubingwa Umekaribia Chelsea,Wameifumua Leicester 3-1 - TodayNews

Breaking

Thursday, 30 April 2015

Ubingwa Umekaribia Chelsea,Wameifumua Leicester 3-1

John Terry scores

Timu ya Chelsea ilibidi wasubiri hadi dakika ya 49 kusawazisha goli kupitia kwa mshambuliaji wake mkongwe mwenye umri wa miaka 38 Didier Drogba,hadi mapumziko Chelsea walikua Yuma kwa goli moja lililofungwa na Marc Albraighton wa Leicester City.Didier Drogba scores
Vijana hao wa Jose Mourinho waliingia kipindi cha pili kwa kasi ya ajabu na kumiliki mpira zaidi na kuwachukua takribani dakika nne kusawazisha goli hilo kabla ya kuongeza tena kupitia kwa kepteni wake John Terry na mwisho kabisa dakika ya 83 alikua ni kiungo Ramires aliepigila msumali wa mwisho.
John Terry celebrates his goal
Kwa matokeo hayo manaake ni kwamba ushindi dhidi ya Crystal Palace jumapili ijayo utakua umewahakikishia wazee wa darajani ubingwa wa msimu huu wa 2014/2015 na kufikisha point 80 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.Ramires scores for Chelsea
Leicester walioonyesha mchezo mzuri na kuongoza kipindi cha kwanza wanabaki nje ya kundi la kushuka daraja kwa pointi moja..

No comments:

Post a Comment