Juventus yaibutua Dortmund 3-0 yatinga Robo fainal kwa jumla ya magoli 5-1 - TodayNews

Breaking

Thursday, 19 March 2015

Juventus yaibutua Dortmund 3-0 yatinga Robo fainal kwa jumla ya magoli 5-1

002c3b2d-938b-47cd-ae5e-bbe9f14e6eea-812x1020Juventus usiku huu wamefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya  kwa jumla ya mabao 5-1 dhidi ya Borussia Dortmund.
Waitaliano hao wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 huku Nyota mwiba wa Juve pamoja na Argentina Carlos Tevez akianza kucheka na Nyavu katika dakika ya tatu kabla ya Morata kupachika bao la pili kunako dakika ya 70.
Kwa mara nyingine tena Tevez akawainua vitini mashabiki wa Juve kwa kutupia kambani bao la tatu katika dakika ya 80.
Kwa matokeo hayo Vibibi vizee hao wanakuwa wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya mchezo wa kwanz a kushinda bao 2-1.
VIKOSI:
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Papastathopoulos, Subotic, Hummels, Schmelzer, Kampl, Bender, Gundogan, Reus, Mkhitaryan, Aubameyang.
Subs: Langerak, Kehl, Kagawa, Blaszczykowski, Kirch, Immobile, Ramos.

Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Vidal, Marchisio, Pogba, Tevez, Pereyra, Morata.
Subs: Storari, Ogbonna, Barzagli, Pepe, Padoin, Llorente, Matri.

Referee: Milorad Mazic (Serbia)
1c3b2de1-7d77-4602-8004-44d99bd8537e-620x372
1426711051894_lc_galleryImage_Juventus_Carlos_Tevez_rig1426711086284_lc_galleryImage_DORTMUND_GERMANY_MARCH_Pa

No comments:

Post a Comment