Klabu ya Mtibwa Sugar imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga Singida United kwa jumla ya mabao 3 – 2 uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Wachezaji waliyo pata kufunga kwa upande wa Mtibwa ni Salum Kihimbwa, Issa Rashid na latatu likifungwa na Ismail Mhesa dakika ya 83 kipindi cha pili wakati kwa upande wa Singida yakifungwa na Salum Chuku pamoja na Tafadzwa Kutinyu.Kwa matokeo hayo sasa Mtibwa Sugar ndiyo itawakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF wakati Simba SC ikiwakilisha upande wa Klabu bingwa Afrika.
Watu wengi walikuwa wanaichukulia poa Mtibwa kwa kulinganisha wachezaji wake na wale wa Singida United, timu ambayo imesajili wahezaji wengi wa kimataifa.
Ukiniuliza Mtibwa waliizidi wapi Singida United kwenye mchezo wa fainali nitakwambia ni uzoefu wa wachezaji waliopo Mtibwa lakini makosa ya golikipa wa Singida United yaliwarahisishia Mtibwa kupata matokeo.



No comments:
Post a Comment