
Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine na pindi unapofikiria kufuga mbwa basi kwanza Jiulize Maswali yafuatayo. Moja Upo tayari kumuhudumia mbwa wako kwenye Chakula, Maradhi, Matibabu, Mafunzo na Kutoa Muda wako wa angalau kuanzia nusu saa mpaka masaa mawili kwaajili ya kukaa nae, kucheza nae na uangalizi? Kama jibu ni HAPANA basi fahamu kuwa hujafikia hatua ya kufuga Mbwa ni heri uache maana vinginevyo yatakuwa mateso kwako na kwa mbwa mwenyewe. Mbwa anahitaji upendo kama ambavyo Binadamu tunavyowapenda binadamu wenzetu na hata kuwahudumia pale wanapokuwa wagonjwa basi na Mbwa ni hivyo hivyo unapoamua kufuga mbwa fahamu ya kuwa naye ni mnyama kama mnyama mwingine ambapo akiumwa anahitaji matibabu. Leo tutaangalia Makundi mbalimbali ya Mangonjwa yanayoweza kumshambulia mbwa, mnyama anayekaribia uhusiano na mbwa, na hata binadamu pia.
Leo tutaangazia Makundi Mawili tu huku Makundi mengine yataangaziwa Katika post zetu zijazo kikubwa ni endelea kufuatilia post zetu kupitia Hapa DOG TIPS TANZANIA ili upate ufahamu na kuweza kutunza vizuri mbwa wako. Kuna aina nyingi ya magonjwa ya mbwa na magonjwa hayo tutayafahamu kupitia katika makundi haya mbalimbali. Makundi hayo Mawilin ni kama yafuatavyo
1: VIRAL INFECTIONS
Viral infections ni magonjwa yanayosababishwa na virusi kutoka kwa mnyama mmoja kwenda kwa mnyama mwingine ambapo magonjwa haya yapo mahususi kwaajili ya mbwa na hata binadamu. Katika Kundi hili la Viral kwa mbwa kuna magonjwa kama vile Rabies (Kichaa cha Mbwa), Canine parvovirus ,Canine coronavirus, Canine distemper ,Canine influenza, Infectious canine hepatitis , Canine herpesvirus , Pseudorabies na Canine minute virus Haya ni baadhi tu ya magonjwa ambayo ni kwaajili ya mbwa lakini pia yapo ambayo yanaweza kumdhuru binadamu pia kama hatochukua tahadhari mapema.
2:BACTERIAL INFECTIONS
Haya ni magonjwa yanayosababishwa na bacteria kama ilivyo kwa wanyama wengine kama binadamu, Magonjwa haya yapo mahususi kwa mbwa na binadamu pia. Katika kundi hili kuna magonjwa kama vile Brucellosis, Leptospirosis, Lyme disease, Ehrlichiosis, Rocky Mountain spotted fever, Clostridium na Kennel cough. Haya ni baadhi ya magonjwa ambayo yanasababishwa na bacteria lakini katika kundi hili pia kuna baadhi ya magonjwa ambayo huweza kumshambulia binadamu kama vile Lyme disease.
3:FUNGAL INFECTIONS
Fungal infections ni magonjwa ambayo husababishwa na fangasi magonjwa haya yanaathiri binadamu pamoja na mbwa japokuwa Mbwa hushambuliwa mara kumi zaidi ya binadamu kwa magonjwa yasababishwyo na fangasi. Magonjwa yasababishwayo na fangasi kwa Mbwa yanaweza kuleta madhara katika Macho, Ubongo, ngozi nk. Katika Kundi hili la magonjwa yasababishwayo na fangasi Ni kama vile Blastomycosis, Histoplasmosis,Coccidioidomycosis,Cryptococcosis,Ringworm,Sporotrichosis,Aspergillosis, Pythiosis pamoja na Mucormycosis.
Katika kundi hili kuna magonjwa baadhi ambayo binadamu anaweza kuyapata na kuathirika na mbwa pia akayapata na kuathirika kama vile Cryptococcosis, Blastomycosis nk.
Haya ni baadhi ya magonjwa ambayo yapo katika kundi hili, Magonjwa haya asilimia kubwa humuathiri Mbwa na kupelekea kuharisha na muda mwingine kupiteza uzito kwa haraka sana
baadhi ya magonjwa hayo katika kundi hili ni kama vile Giardiasis, Coccidiosis, Leishmaniasis, Babesiosis, Protothecosis pamoja na Neosporosis.
No comments:
Post a Comment