Jua Aina Kumi za Mbwa - TodayNews

Breaking

Friday, 1 June 2018

Jua Aina Kumi za Mbwa

1: Affenpinscher

Affenpinscher ni aina flani hivi ya mbwa ambao hupatikana sana ndani ya Nyumba za watu ambao wanapenda kampani ya mnyama huyu.Aina huwa na Umbo dogo kama ambavyo anaonekana katika picha.





2:Germany Shepherd Dog

Aina hii ya Germany Shepherd imekuwa maarufu sehemu mbalimbali za dunia hususani Tanzania ambapo wengi wanawafahamu hawa mbwa kama Mbwa wanaotumiwa na Jeshi la Polisi kitengo cha Mbwa. Mbwa hawa asili yao ni Ujerumani. 


3: BoerBoel:

Aina hii inajulikana kwa jina la BoerBoel ambapo asili ya Mbwa hawa ni huko Afrika Kusini, Mbwa huyu anamuonekano unaotaka kufanana na simba, na ni aina flani ya mbwa ambae ana umbo kubwa na lenye mvuto. 




4: Doberman Pinscher

Mbwa huyu anaitwa Doberman Pinscher ambae asili yake ni Ujerumani pia Lakini mbwa huyu inasemekana ni moja kati ya mbwa hatari sana.

 
5:Rottweiller

Huyu anaitwa Rottweiller ambae pia asili yake ni huko Ujerumani, Mbwa huyu kwa Tanzania anafahamika kama Macho manne kutokana na vidoti viwili alivyonavyo juu ya macho yake. Ni mbwa mmoja mzuri sana lakini anayehitaji uangalizi wa hali ya juu 


6:Belgian Mallinois

Mbwa huyu anaitwa Belgian Mallinois ambae asili yake ni nchini Ubeligiji Mbwa huyu anatumika sana na Majeshi katika Nchi mbalimbali kama vile Ujerumani, Marekani na kwingineko, Huku kwetu hajaweza kuwa maarufu sana lakini pia wengi hawamfahamu na wakimuona basi umfananisha na Germany shepherd na kumpa jina hilo ilhali sio kweli.



7:Maltesse

Aina hii inaitwa Maltesse ambapo kwetu Tanzania hupenda kusema mbwa wa mapambo ambae wengi husema huyu kazi yake sio kulinda.



8:Great Dane

Huyu ndio Great Dane mbwa hawa wameanza kushika hatamu katika nchi yetu ya Tanzania ambapo sasa wafugaji wengi wameanza kuwa nao kutokana na Umahiri wake katika nyanja mbalimbali kama ulinzi.



9:Cane Corso

Huyu anaitwa Cane Corso ukimuangalia vibaya unaweza sema ni BoerBoel kumbe sio Huyu asili yake ni Nchini Italia. 



10:American Pit Bull Terrier

Anaitwa American Pit Bull Terrier mbwa huyu inasemekana ndio mbwa hatari kabisa kuliko mbwa aina nyingine lakini bado kuna mijadala mingi inayosema kuwa mbwa huyu ni hatari zaidi kuliko wengine huku wengine wakisema sio.


No comments:

Post a Comment