KIUNGO wa Barcelona, Philippe Coutinho, amesema kwamba anavyoamini mastraika Mohamed Salah na Neymar watatisha katika fainali za Kombe la Dunia zikazoanza hvi karibuni nchinniu Urusi.
Wawili hao wanatarajia kwenda katika mashindano hayo wakiwa majeruhi, baada ya Salah kuumia bega katika mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa na huku Neymar akiwa jacheza muda mrefu baada ya kuvunjika mguu Februari mwaka huu.
Hata hivyo, Coutinho, ambaye aliwahi kucheza na Salah wakiwa Liverpool kabla ya Januari mwaka huu kuhamia Barcelona na ambaye amekuwa akicheza na Neymar katika safu ya ushambuliaji ya timu ya Taifa ya Brazil, anasema kuwa mastaa hao wanaweza kuwafunika hata Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakati wa fainali hizo.
“Kwa sasa nadhani ni mawazo ya kila mmoja kufanya vizuri wakati wa fainali za Kombe la Dunia,”alisema Coutinho.
“Messi na Ronaldo wamekuwa wakitamba kwa miaka mingi. Nadhani sasa ni wakati wa wachezaji wengine kufanya vizuri duniani na katika fainali za Kombe la Dunia,”alisema staa huyo.
“Kwangu mimi, Salah na Neymar wana nafasi kubwa ya kufanya hivyo. Ingawa itategemea na jinsi mashindano yatakavyokwenda, lakini wana kipaji cha kufanya hivyo,”alikwenda mbali zaidi nyota huyo.
No comments:
Post a Comment