Ufaransa wapiga marufuku mikusanyiko wakati wa kombe la dunia - TodayNews

Breaking

Wednesday, 30 May 2018

Ufaransa wapiga marufuku mikusanyiko wakati wa kombe la dunia


Matumaini ya mashabiki wa timu ya soka ya Ufaransa kuitizama timu yao katika sehemu za wazi ‘public viewing” yamekufa baada ya serikali nchini humo kushirikiana na chama cha soka AFP kupiga marufuku.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchini humo ameshawatangazia kwamba miji inayojipanga kuonesha mashindano ya kombe la dunia katika sehemu za wazi inabidi iachane na mpango huo kwani umezuiliwa.
Sababu kubwa ya kuzuia jambo hili ni kutokana na matishio ya kigaidi, ikumbukwe kwamba nchi ya Ufaransa ni moja ya wahanga wakubwa wa matukio ya kigaidi ambayo mengi siku za karibuni yamefanywa sehemu za wazi.
Mwaka jana kulitokea shambulizi katika kituo cha reli nchini ambapo watu kadhaa walifariki na mwaka huu pia mwezi March kulitokea shambulizi la bunduki katika kitongoji cha Trebes nchini Ufaransa.
Ufaransa wanakwenda katika michuano hii kwa mara ya 14 huku wakiwa wamebeba kombe hilo mara moja, Ufaransa safari hii wako katika Group C pamoja na timu za Dernmark, Peru na Australia.

No comments:

Post a Comment