Scholes amewakosoa MO Salah na Karius - TodayNews

Breaking

Wednesday, 30 May 2018

Scholes amewakosoa MO Salah na Karius

May 26 2018 ulichezwa mchezo wa fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool nchini Ukraine katika mji wa Kyiv na Liverpoolkujikutana wakikubali kipigo cha magoli 3-1.


Mchezo huo ulimalizika kwa kipa wa Liverpool Loris Karius kukutana na lawama baada ya kuruhusu kufungwa magoli mawili yanayodaiwa kuwa yakizembe, ambayo pia yamechangia kuidhoofisha Liverpool kwa kiasi kikubwa.



Kiungo wa zamani wa Man United Paul Scholes amewakosoa Loris Karius na Mohamed Salah kwa kitendo chao cha kulia, Karius alilia baada ya kuhisi amewaangisha timu hukuSalah alilia wakati akitolewa nje ya uwanja dakika ya 25 kwa kuumia bega baada ya kuvutana na Sergio Ramos.
“Naweza kumuelewa Karius kwa kilichotokea kuwa kinaumiza lakini sio kufikia kulia, kuhusu Salah majeruhi ni sehemu ya mchezo, miaka iliyopita ukiona mchezaji analia ujue ina maana kubwa sana lakini kwa sasa ni tofauti wachezaji wanalialia tu kirahisi”>>>Scholes.
“Binafsi tumeshwahi kupoteza fainali kadhaa najua inaumiza lakini kufikia kulia? hapana sikumbuki kama nimeshawahi kulia katika soka labda nikiwa na umri wa miaka 11 au 12 tukiwa tumepoteza game za fainali”

No comments:

Post a Comment