Ajali ya Meli yaua watu zaidi ya 50 DRC - TodayNews

Breaking

Sunday, 27 May 2018

Ajali ya Meli yaua watu zaidi ya 50 DRC




Maiti zaidi ya hamsini zimeopolewa baada ya meli moja kuzama Jumatano wiki hii katika mto mmoja kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa takwimu za serikali.
Ajali hiyo imetokea katika mto Tshuapa Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
"Sababu za ajali hiyo na idadi ya watu ambao hawajapatikana haijajulikana. Ujumbe kutoka kwa serikali ya mkoa huo tayari umetumwa katika eeneo la tukio kujua hali halisi ya mambo," Bw Mboyo ameongeza.
Ajali kama hii zinatokea mara kwa mara nchini DRC, kwenye maziwa au kwenye mito, na ajali hizi mara nyingi zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi.
Mnamo mwezi Februari, watu zaidi ya kumi na nne walikosekana katika ajali ya meli mbeli zilizozama katika Mto Congo.

No comments:

Post a Comment