WACHEZAJI HAWA MIKATABA YAO INAISHA MWISHONI MWA MSIMU HUU. - TodayNews

Breaking

Tuesday, 17 November 2015

WACHEZAJI HAWA MIKATABA YAO INAISHA MWISHONI MWA MSIMU HUU.

Ibrahimovic 1Zlatan Ibrahimvoc
Amekuwa na klabu ya PSG kwa kipindi cha miaka 3 sasa tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2012 akitokea klabu ya AC Milan ya nchini Italia.
Mchezaji huyo amenukuliwa akisema kuwa “ameziweka nchi za Sweden na Ufaransa katika ramani ya soka”.Vilabu vingi vimehusihwa kumtaka mchezaji huyo vikiwepo vilabu vya Manchester United,Ac Milan na Inter Milan.
Kwa sasa Zlatan Ibrahimovic ana miaka 34.
xabi alonso 1Xabi Alonso
Kwa sasa anaichezea klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.Xabi amevichezea vilabu vikubwa kama Liverpool na Real Madrid kabla ya kujiunga na Bayern mwaka 2014 kwa mkataba wa miaka miwili.
Mpaka sasa klabu ya Bayern Munich ipo kimya kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo. Xabi ana miaka 33 na tarehe 25 mwezi huu anafikisha miaka 35.
Michael CarrickMichael Carrick
Amekuwa msaada mkubwa na amepata mafanikio makubwa katika klabu ya Manchester United.Carrick alijiunga na Manchester United mwaka 2006 akitokea klabu ya Tottenham Hotspur.
Kuna kila dalili ya Carrick kuongezewa mkataba mpya na klabu ya Manchester United lakini mkataba wake wa sasa unaisha mwaka 2016.
Michael Carrick kwa sasa ana miaka 34.
terry 2John Terry
Ameitumikia klabu ya Chelsea katika maisha yake yote ya soka.Kwa sasa ana miaka 34 na mwezi ujao atafikisha miaka 35.
John Terry ni mmoja kati ya mabeki bora wa kati duniani lakini amekuwa katika wakati mgumu msimu huu kutokana na kucheza chini ya kiwango.Mkataba wa Terry unamalizika mwakani 2016.
Wachezaji wengine wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu ni pamoja na;
Patrice Evra(Juventus),Victor Valdes(Manchester United),Branislav Ivanovic(Chelsea),Ezequel Lavezzi(PSG),Naldo(Wolfsburg),Martin Demichelis(Manchester City),Hatem Ben Arfa(Nice)

No comments:

Post a Comment