Yanga, Simba zisicheze kwa kuogopana - TodayNews

Breaking

Sunday, 8 March 2015

Yanga, Simba zisicheze kwa kuogopana



LEO, Jumapili mahasimu wa soka nchini Simba na Yanga watajitupa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara.
Katika mechi ya kwanza ya ligi hiyo, timu hizo zilitoka suluhu na kuishia kugawana pointi.
Kwa kawaida mechi za Yanga na Simba hamasa yake huwa kubwa kuliko mechi nyingine yoyote ya Ligi Kuu na ndio maana haishangazi kuona timu zote zimelihama jiji la Dar es Salaam kwa muda.
Yanga wameweka kambi Bagamoyo mkoa wa Pwani wakati Simba wamekwenda kujichimbia visiwani Zanzibar.
Zipo sababu nyingi zinazohusishwa na hatua ya klabu hizo kulihama jiji, moja kati ya hizo ni hujuma, hofu kwamba wachezaji wao wanaweza kuhujumiwa lakini pia ukubwa wa mechi ni ukweli ambao hauwezi kuwekwa kando.
Ukubwa wa mechi yenyewe unazifanya timu hizo kufanya maandalizi ya kina likiwamo kwenda maeneo ya mbali ambako wachezaji na makocha wataweka mkazo katika suala zima la mazoezi.
Ukiachana na maandalizi ya timu hiyo, mechi hizi pia ni wakati wa mavuno kwa baadhi ya wanachama na mashabiki ambao huneemeka kutokana na viingilio.
Tuliwahi kuzungumzia katika ukurasa huu juu ya umakini wa kudhibiti wanaohujumu mapato ya mechi na tunadhani jambo hilo linatakiwa kufanyika kesho.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liweke mkakati wa kuwadhibiti wezi ambao walishindwa kuhujumu mapato wakati mfumo wa tiketi za elektroniki ukitumika.
Ni kweli kwamba mfumo wa tiketi za elektroniki umekuwa na matatizo lakini ndio mfumo wa kisasa ambao tunaamini matatizo yaliyojitokeza yakitatuliwa ndio utakaokuwa ukitumika.
Ukiachana na hilo yapo mazowea ya wachezaji kucheza kwa kuogopana katika mechi hii..
Imekuwa kawaida wachezaji kucheza chini ya viwango vyao au kucheza katika namna ya kujihami zaidi hali inayoufanya mchezo ukose burudani inayokusudiwa.

No comments:

Post a Comment