Sababu zilizomfanya mkali Diego Costa Kuitosa Liverpool 2013 - TodayNews

Breaking

Friday, 6 March 2015

Sababu zilizomfanya mkali Diego Costa Kuitosa Liverpool 2013

Diego Costa

 Diego Costa mshambuliaji kutoka katika timu ya Chelsea ya Uingereza ameweka wazi kuwa ilikuwa imebakia kidogo tu ajiunge na kikosi cha majogoo wa wa Anfield, Liverpool FC kwa mwaka 2013, wakati walipoandaa ofa ya paundi mil 21 kwaajili ya kumsaini, Jarida la The Star liliripoti.
Mshambuliaji huyo wa kati kutoka Hispania wakati huo alikuwa na timu ya Athletico Madrid alipata ofa hiyo ya kujiunga na Liverpool kupitia manager wake Breandan Rodgers lakini ilishindikana kutokana na Diego kuwa kama namba tegemezi katika timu ya Athletico
Costa aliona kama amekuwa namba nzuri zaidi na mlengwa zaidi kwa wakati huo kuwa na timu hiyo ya Kispaniola na kupelekea kutotengeneza mkataba na Liverpool na isitoshe yeye alikuwa kama namba pekee kwenye nafasi ya ushambuliaji iliyoshika namba moja kama alivyojihakikishia.
Diego Costa ilimbidi tu abaki na waspain hao na ilimpelekea kumaliza msimu mzima wa ligi kwa kutia kambani magoli 27 na kukiwezesha kikosi hicho cha Diego Simeon kubeba taji la La Liga au Ligi kuu ya Sapin. Diego Costa alifanikiwa pia kucheza kombe la UEFA kwa wakti huo na kufika hadi fainali ambayo haikuwa nzuri kwao mara baada ya kupata kipondo cha goli 4-1 kutoka kwa Real Madrid timu ambayo ilikuwa katika kiwango bora zaidi huku wakishinda baada ya dakika 90  za uwanjani (extratime).
Diego Costa alisema kuwa alikubali kupokea ofa toka Liverpool
” Nilikuwa tayari kuondoka, Liverpool ni timu kubwa sana, lakini baada ya kujituma zaidi na timu yangu ya Athletico huku nikijihakikishia namba ningeondoka vipi?
Nadhani ilikuwa wakati mwafaka zaidi kuendelea kukulia pale na kuitumikia timu yangu huku nikicheza kwa miaka mingi zaidi na zaid” Costa alisema.
Costa alifanikiwa kujiunga na Chelsea kwa takribani paund mil 32 msimu wa mwisho wa majira ya kiangazi na hadi sasa akiwa na magoli 17 akiwa na Chelea.

No comments:

Post a Comment