Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili dhidi ya Stoke city jumapili iliyopita
GWIJI wa the gunners HENRY amemtabiria mazuri Alexis Sanchez akitangaza kuwa nyota huyo raia wa Chile atakuwa mrithi wa kufumania nyavu Emirates.
Sanchez ameanza kwa makali katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu England na siku ya jumapili iliyopita Arsenal ikishinda 3-0 dhidi ya Stoke city alikuwa moto wa kuotea mbali na alitia kambani gozi la ng’ombe.
Uwezo wake wa kumalizia pasi za mwisho,kufunga na kasi yake ya umeme kumesababisha watu wamfananishe na Henry, mshambuliaji mkubwa katika historia ya klabu hiyo. Mfaransa huyo anaamini kumfananisha yeye na Sanchez ni sahihi.
No comments:
Post a Comment